Clattenburg hatafunguliwa mashtaka-FA
22 Novemba, 2012 - Saa 17:28 GMT

Mark Clattenburg
Shirikisho la mchezo wa soka
nchini Uingereza FA limetangaza kuwa halitamfungulia mashtaka yoyote
refa Mark Clattenburg, ambaye anatuhumiwa kutumia lugha ya ubagusi dhidi
ya mchezaji wa Chelsea, wakati wa mchuano wa mechi ya ligi kuu ya
premier ya England.
Mcheza kiungo wa Chelsea, Ramires, alidai kuwa
alisikia refa huyo akimueleza mchezaji mwingine wa Chelsea John Obi
Mikel, Nyamasa nyani huyo wakati wa mechi yao tarehe 28 mwezi uliopita
dhidi ya Manchester United katika uwanja wa Stamford Bridge.Lakini shirikisho hilo limesema kuwa hakuna ushahidi wa kutosha ili kumfungulia mashtakab refa huyo.
Comments
Post a Comment